Unadhani itakuchukua muda
gani kuamua rangi ya/(za) harusi au sherehe yako? Je unazo sababu kwanini
umechagua rangi hizo na si nyinginezo? Je ungependa kuifanyia sherehe yako
sehemu gani na kwanini? Décor je? Ni kitu gani unahisi kitakuwa cha tofauti sana
kati yako na harusi ya mtu mwingine yeyote uliyohudhuria hivi karibuni?
Nyakati zimepita ambapo
harusi ilikuwa tu ni siku ya kualika ndugu na jamaa wakae nawe, muende kupiga
picha za ukumbusho photo-point, mle na kunywa na kutoleana zawadi halafu kila
mtu arejee kwao. Hizi ni zama za kuweka ‘class’ na utofauti (uniqueness) kwenye
sherehe/harusi yako…wapatie watu sababu ya kuikumbuka harusi/sherehe yako hata
baada ya miaka 5 ijayo..kuanzia kwenye uchaguzi wa rangi, designing, location
ya sherehe, urembaji (decors),…na meengi mengineyo!....
Nimeshawishika kuweka hapa
picha za harusi hii kati ya mtanzania Bw. Nathan Chiume na mrembo Jerryanne
Heath raia wa Jamaica iliyofanyika huko New
York…Picha za harusi hii zikiwa zimepigwa na Petronella Photograghy..embu
jionee..
Pete yenye madini ya Tanzanite!!……ladies ni kama ninaona mnavyotoa macho na kutamani…..
Nathan na Anne wanadai kuwa waliamua kuchagua rangi za blue bahari na njano kwa sababu huwakumbusha kuhusu bahari na jua…je ni kwanini wewe ulichagua rangi za harusi yako?
Wawili hawa waliichagua siku yao ya harusi (June 21, 2013) sababu ni summer solstice, siku ambayo huwa ndefu kuliko siku nyingine zote za mwaka (kumbuka Jiografia..ha ha)
Pamoja na mambo mengine,
ukumbi ulikubali kuweka kila kitu ikiwamo vyakula katika machaguo ya maharusi
hawa…
Urembo ulionakshiwa na utamaduni
wa kiafrika..hii ilikuja baada ya Nathan na Anne kutembelea Tanzania na Jamaica
kuliko na asili yao, na kupata vionjo hivyo vinavyoonekana…